USULUHISHI

Je ni njia gani tunatumia kutatua migogoro kuhusu majina ya vikoa vya .tz?


Utatuzi wa migogoro husuluhishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za tzNIC
Mtu yeyote anayesajili jina la kikoa cha .tz kupitia wakala anayeaminika, moja kwa moja anakubaliana, kupitia fomu ya makubaliano, na sheria na taratibu zote za usajili wa majina ya vikoa zinazosimamia shughuli zote za kikoa cha .tz
Sheria ya kumaliza migogoro ni moja kati ya sheria zilizomo kwenye muongozo mkuu na ina lengo kuu la kupambana na wizi wa majina maarufu ya vikoa/ usajili usio halali wa majina ya vikoa maarufu na kuyauza kwa lengo la kujipatia faida. Sheria hii inakulinda na namna zifuatazo za usajili:

  • Jina la kikoa linalofanana na lingine na hivyo kuleta mkanganyiko
  • Matumizi halali ya jina la kikoa
  • Matumizi ya jina la kikoa kwa sababu ovu

Kwa sasa WIPO ni tzNIC's DRS , wanatoa huduma ya haraka isiyo na gharama ya utatuzi wa migogoro kwa taasisi na kampuni zote zilizosajiliwa chini ya .tz. Sheria na taratibu zinazotumika kutatua migogoro hiyo ni kwa mujibu wa sheria na taratibu za tzNIC pamoja na sheria nyingine za ziada zilizowekwa na msimamizi.