Jinsi ya kusajili jina la kikoa cha .tz

Ili kukurahisishia wewe namna ya kusajili jina la kikoa cha .tz, tzNIC inakupa njia mbili rahisi :

  • Tukiwa na zaidi ya mawakala 40 wanaoaminika nchini kote, unaweza ukasajili jina la wavuti wako kwa urahisi kabisa kwa shilingi elfu 25 za Kitanzania ama dola za Kimarekani 30. Pata faida mara mbili kwa kusajili jina la kikoa chako na kuhodhi jina la wavuti wako kwa mawakala wetu wanaoaminika. Tunakushauri sana uwatumie mawakala wetu kwani ni njia rahisi na nafuu zaidi ya kujisajili na kuendesha wavuti wako
  • Lakini pia unaweza kusajili jina la kikoa chako moja kwa moja nasi ijapokuwa hatukushauri sana ufanye hivi. Endapo utaamua kuchagua njia hii, itabidi uwe na ujuzi kiasi wa masuala ya kiufundi. Ili uweze kujisajili ni lazima utoe anuani mbili za IP za majina ya seva ambayo yapo kwenye mtandao wa intaneti saa ishirini na nne pamoja na kulipa kiasi cha shilingi elfu 45 za kitanzania. Kusajili kikoa chako nasi jaza fomu hii na kuituma