KUWA WAKALA WETU
Unataka kuwa wakala wetu?

 • Ongezea faida biashara yako ya kuhodhi wavuti na usanifu kwa kuwa mmoja wa wakala anayeaminika wa .tzNIC
 • Unaweza kusajili majina ya wavuti muda wowote kwa kupitia mfumo wetu
 • Ongeza wigo wa biashara yako kwa kuuza haki za kuhodhi wavuti kwa watu wengine

Vigezo vya kuwa wakala

 • Una usajili halali wa kibiashara na ofisi maalum iliyopo katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 • Unakubaliana na vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye nyaraka za .tzNIC
 • Uzoefu uliothibitishwa wa kusimamia seva za mfumo wa majina ya wavuti (DNS)
 • Uwezo wa kusajili majina ya wavuti kupitia mfumo wa FRED unaosajili majina ya vikoa vya .tz

Mchakato

 • Jaza kwa usahihi fomu kwa ajili ya kuwa wakala na mkataba wa msajili.
 • Peleka ukapigwe muhuri na wakili.
 • Usisahau kuambatanisha nyaraka zote husika kama zilivyoainishwa kwenye fomu ya maombi, kwa mfano cheti cha biashara, wasifu wa kampuni yako, orodha ya wafanyakazi wa kampuni yako n.k
 • Tuma fomu ya maombi pamoja na nyaraka zote husika kwenye ofisi za .tzNIC (waweza kwenda mwenyewe, au ukatumia njia ya posta ama kwa barua pepe) copy );

.tzNIC itafanyia tathmini maombi yako na kukupa mrejesho baada ya wiki moja