tzNIC kuendesha warsha ya huduma za vikoa vya .tz, Dar es Salaam

Kwa kushirikiana na shirika linalosimamia uendeshaji wa Intaneti duniani (ICANN), Rajisi ya .tz (tzNIC) itaendesha warsha ya siku 2 (10 & 11 Desemba 2015) katika kumbi za mikutano za Benki kuu (BOT).

Lengo la warsha hii ni kutoa fursa kwa wadau mabalimbali wa Intaneti kubadilishana uzoefu katika kuongeza matumizi ya majina ya vikoa vya .tz hapa nchini. Warsha hii inafanyika katika kipindi ambacho takribani majina ya vikoa vya nchi za Afrika millioni 1.3 tu yanatumika katika bara la Afrika lenye zaidi ya wakazi Billioni 1!

Kati ya mambo yatakayojadiliwa katika warsha hii ni pamoja na:
a) Nini kifanyike ili majina ya vikoa vya nchi yaweze tumika kwa wingi barani Afrika?
b) Rajisi (registry) na wasajili (registrars) wafanye jitihada gani ili kukukuza biashara na matumizi ya majina ya vikoa vya .tz hapa nchini?
c) Nini chapaswa kufanywa na wadau wengine kusaidia kukuza biashara na matumizi ya majina ya vikoa vya .tz?

Ratiba ya warsha inapatikana hapa