Sisi ni nani?

Kituo cha mitandao cha Tanzania (tzNIC) ni wakala wa usajili wa mitandao kwa ajili ya majina ya vikoa vya .tz. Tunaratibu mfumo mzima ambao unaweza ukatambua barua pepe ama wavuti zenye usajili wa .tz.


Kwa kupitia mchakato wa majadiliano, kituo cha mitandao cha Tanzania, ni kampuni isiyo ya kibiashara iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 ili kuweza kuratibu na kusimamia shughuli mbalimbali za ccTLD. tzNIC ni kampuni tanzu iliyoanzishwa na TCRA, ambao ni wasimamizi, na TISPA, ambao ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali za utoaji huduma za intaneti.

Dhima:
Kukuza matumizi ya majina ya wavuti yenye usajili wa .tz na kulinda maslahi ya kampuni ama taasisi zilizojisajili kwa kuwahahakikishia mfumo salama kabisa wa usajili wa vikoa vya .tz lakini pia kuwapatia wateja majina ya vikoa kwa gharama nafuu.


Dira:
Kuwa moja ya wasajili wa vikoa bora na wanaoaminika duniani kote