Kuhusu sisi

Kituo cha mitandao cha Tanzania (tzNIC) ni wakala wa usajili wa mitandao kwa ajili ya majina ya vikoa vya .tz. Tunaratibu mfumo mzima ambao unaweza ukatambua barua pepe ama wavuti zenye usajili wa .tz.


Kwa kupitia mchakato wa majadiliano, kituo cha mitandao cha Tanzania, ni kampuni isiyo ya kibiashara iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 ili kuweza kuratibu na kusimamia shughuli mbalimbali za kikoa cha .tz. tzNIC ni kampuni tanzu iliyoanzishwa na TCRA, ambao ni wasimamizi, na TISPA, ambao ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali za utoaji huduma za intaneti